Waswahili usema usitupe cha zamani kwa kupata kipya ni kweli au ni
msemo tu, kama ni msemo basi Snura Mushi mwigizaji na mwanamuziki wa
kizazi kipya anatiririka kuhusu muziki na filamu, kwa sasa mwanamuziki
huyo anasema kuwa muziki anaufurahia kwani mawazo yake yanafanya kazi.
“Najua katika upande wa muziki nimeshika nafasi nguvu zangu nafikiria
kuhamishia katika filamu kwani ndio fani iliyonitambulisha, shida
ukicheza sinema za watu unashindwa kuwakilisha mawazo yako, nitafanya
katika filamu yangu,”
Msanii huyu anayetamba na wimbo wake wa Chura anasema kuwa yeye ni
mbunifu na mtunzi mzuri wa filamu hivyo punde akitengeneza filamu yake
itakuwa na viwango vya kimataifa tofauti sasa anaposhiriki sinema za
watu anabanwa kuonyesha kitu tofauti
0 comments:
Post a Comment