Indiana. Seneta wa Jimbo la Texas, Ted Cruz amejiondoa katika kinyang’anyiro cha uteuzi kugombea urais wa Marekani kupitia Chama cha Republican. Hatua hiyo imeacha njia nyeupe kwa mgombea Donald Trump.
Cruz alifikia uamuzi huo huku zikiwa zimebaki siku 166 kufanyika Uchaguzi Mkuu Marekani huku wagombea wakiendelea kutafuta kura za maoni kwa ajili ya kuteuliwa na vyama vyao kuwania nafasi hiyo nchini humo.
Chanzo cha kujitoa kuwania nafasi hiyo kinaaminika kwamba ni baada ya Cruz kubaini kupoteza kura katika kampeni za mwisho katika jimbo la Indiana.
Cruz aliwaambia wafuasi wake kuwa alifanya kila aliloliweza katika kampeni zake, lakini hakuona uwezekano wowote wa yeye kuweza kusonga mbele zaidi ya kuamua kujitoa katika kinyang’anyiro hicho.
Baada ya kutangaza kujitoa kwa mgombea huyo machachari katika vituo vya kupigia kura Indiana, wafuasi wake walistushwa ikiwa ni pamoja na kukatishwa tamaa.
Ilidaiwa kwamba tangazo hilo linatoa mwanya kwa Donald Trump kupata uteuzi wa chama chake cha Republican. Wengi wamekuwa wakisema kuwa Seneta Ted Cruz ndiye pekee aliyekuwa anaweza kumshinda Donald Trump kwenye uteuzi wa chama cha Republican.
Cruz ambaye ni seneta kutoka jimbo la Texas, tayari alionyesha dalili mapema baada ya kuibuka mshindi katika uteuzi wa jimbo la Iowa. Lakini katika hatua ya kushangaza, alijitoa kwenye kinyang’anyiro baada ya kushindwa kwenye mchujo jimbo la Indiana. Kura hizo zilionyesha kwamba Trump ameibuka na kura asilimia 57.3 huku Cruz akipata kura asilimia 36.6.
‘’Usiku huu nasikitika kusema kwamba nimeamua kujitoa kwenye kinya’nganyiro hiki ’’nashukuru kwa ushirikiano wenu raia wa hapa Indiana ni ngumu sana kusema lakini naamua kujitoa’, ’ alisema Cruz
Historia
Rafael Edward Cruz alizaliwa mwaka 1970 eneo la Calgary nchini Canada suala ambalo lilidaiwa huenda lingetumiwa na wapinzani wake kumpinga.
Mama yake alikuwa raia wa Marekani jambo lililompa uraia mara mbili wa nchi hizo huku baba yake akiwa ni mhamiaji kutoka Cuba. Baba yake huyo aliingia Marekani kukimbia utawala wa Batista.
Familia ya Cruz ilihamia Houston huko Texas mwaka 1974 ambako akiwa na umri wa miaka mitatu alipewa jina Ted.
Alihudhuria masomo yake katika Chuo Kikuu cha Prince ambako alikuwa maarufu wa midahalo na kisha kujiunga na Chuo cha Harvad kusomea sheria.
Cruz alihudumu kama karani wa mkuu wa sheria katika Mahakama Kuu mwaka 1996 na kujiunga na kampuni ya masuala ya sheria mjini Washington DC ambako alikuwa akishughulikia kesi kubwa. Alikutana na mkewe, Heidi Nelson wakati wote hao walikuwa washauri kwenye kampeni ya George W Bush mwaka 2000 na kubarikiwa kupata watoto wawili wasichana.
2012 aligombea useneta katika jimbo la Texas dhidi ya mgombea maarufu. Hata hivyo, aliibuka mshindi na ndiyo wakati wa kwanza Cruz kushikilia ofisi ya umma.Cruz alitangaza azimio lake la kugombea urais mwaka 2016 katika Chuo cha Christian Liberty.
Aliahidi kuwarudisha watu makwao na kuboresha usalama katika mpaka wa Marekani na Mexico.

Cruz ,Bush waliungana
Machi 24, aliyekuwa mtiania katika mchakato wa uteuzi kumpata mgombea urais wa Marekani, Jeb Bush alitangaza kumuunga mkono Cruz katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa Republican.
Bush, alitangaza kumuunga mkono aliyekuwa hasimu wake wakati chama hicho kinakabiliwa na mgogoro wa ndani kuhusiana na mafanikio ya Trump.
Bush alilaumu matamshi na mbinu chafu za kukigawa chama vinavyotumiwa katika kampeni za Trump, ambavyo ni miongoni mwa mambo aliyoyasema ni kujenga ukuta kati ya mpaka wa Marekani na Mexico na kuzuia Waislamu wasiingie Marekani.
Bush alijitoa katika kinyang’anyiro cha kuwachuja mgombea urais kupitia Republican baada ya kufanya vibaya katika mchujo uliofanyika majimbo ya Lowa, Hampshire na South Carolina.

0 comments:
Post a Comment