Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa
habari wakati alipotembelea kituo cha Mabasi yaendayo haraka cha Kamata
Kariakoo jana, amesema kuwa kuanzia jumatatu Mei 16, 2016 ndio nauli za
mabasi ya mwendo wa haraka zitaanza kutozwa.
Pia
amewaasa watumiaji wa barabara hasa watembea kwa miguu, baiskeli na
maguta wasitumie barabara hizo ili kuepusha usumbufu kwa madereva wa
mabasi ya mwendo wa haraka.
Amesema
ameamua kuongeza muda wa kuanza kutoza nauli hizo kwa watumiaji wa
mabasi hayo kwaajili ya kuelimisha wananchi namna ya kukata tiketi na
jinsi ya kuzitumia wakati wanapoingia kwenye kituo kwaajili ya kusubiri
magari.
0 comments:
Post a Comment