Tangu
kuanza kwa zoezi la kufuatilia wafanyabiashara wanaoficha sukari kwa
agizo la Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Dr John Pombe Magufuli,
kumekuwa na wimbi la watu wanaojiita “makachero wa TAKUKURU kutoka Makao Makuu” nao wakifuatilia sakata la sukari mkoani Kilimanjaro.
Matapeli
hao ambao kwa sasa wapo wilayani SIHA, wamekuwa wakiwasumbua
wafanya biashara kwa kudai kuwa wametumwa kuwashughulikia huku wakiomba
kupewa fedha ili wawasafishe.
Kiasi
cha fedha ambacho kimekuwa kikiombwa ni kati ya Shilingi 150,000/= hadi
500,000/= kama “gharama ya kuwasafisha kwa Mheshimiwa Rais”
Naomba
wafanya baiashara Mkoani Kilimanjaro waelewe kwamba, TAKUKURU inao
mfumo wa utendaji kazi ambao unajali misingi ya utawala bora na kamwe
haihusiki na utapeli wa aina hii.
TAKUKURU
katika utendaji wake wa kazi, haiwatozi wafanya biashara fedha kama
adhabu kwa kuhifadhi sukari kinyume na taratibu. TAKUKURU inafuatilia,
kuhoji na kumtaka mfanyabiashara kuonesha namna anavyomiliki sukari
hiyo kwa kutoa vielelezo husika. Mwisho wa zoezi hili, atakayetoa tamko
ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Ifahamike
kuwa hakuna afisa wa TAKUKURU mpaka sasa aliyetumwa kutoka Makao Makuu
kuja mkoani Kilimanjaro kufuatilia zoezi la sukari. Zoezi hili mkoani hapa linaendeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama kama timu moja na wala halifanywi na TAKUKURU pekee .
Ifahamike pia kuwa hakuna zoezi linaloihusisha TAKUKURU litakaloendeshwa mkoani bila ofisi ya mkoa kuwa na taarifa.
Kwa
misingi hiyo yeyote anayeendesha zoezi hilo nje ya utaratibu
nilioufafanua ni tapeli, taarifa zake zitolewe mapema ili akamatwe na
kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Maofisa
wote kutoka ofisi ya TAKUKURU mkoa wanavyo vitambulisho na kama
watatiliwa shaka basi ofisi yangu ijulishwe kupitia simu namba 0784
998 804 au 0786 089 805 muda
wowote.
IMETOLEWA NA
ALEX J KUHANDA
MKUU WA TAKUKURU MKOA WA KILIMANJARO
11/5/2016.
0 comments:
Post a Comment