Monday, May 2, 2016

Meya wa Kinondoni Agawa Bure Maeneo ya Biashara Leo na Kufuta Umiliki wa Vibanda na Vizimba 100

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Mstahiki Boniface Jacob amezua taharuki kwa wamachinga wa ubungo na kukimbia biashara zao wakiambatana naye mithili ya Maandamano mara baada ya kutangaza kufuta umiliki wa vizimba na mabanda takriban 100 yaliyokuwa yakimilikiwa na watendaji na Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni katika soko la Mawasiliano Maarufu kama Simu 2000 akiagiza wapewe bure.
Mstahiki Jacob aliyefuatana na watendaji wa Manispaa hiyo alitembea kwa miguu akiongea na wamachinga mmoja mmoja na makundi kuanzia Ubungo Plaza hadi ubungo maji akiwaelimisha umuhimu wa oparesheni ya kuwaonda barabarani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa njia za juu na kuanza kwa usafiri wa mabasi ya kasi Dart ambao hali ilibadilika pale alipotaja Manispaa kuwa na masoko 26 yaliyohodhiwa na viongozi kwa kuingia Mikataba ya kupangisha wakati wamejiagawia bure.

Aidha Mstahiki Meya Boniface Jacob amesema katika kuhakikisha wafanyabiashara wadogo wanatengewa maeneo yao watafanya uhakiki katika masoko yote kubaini viongozi na watendaji waliojimilikisha na kuwanyang’anya ili masoko yatumiwe na walengwa ikiwa ni hatua ya kuboresha mazingira ya jiji huku mtendaji wa kata ya ubungo Bw. Gilbati Mushi akieleza hatua hiyo kudhihirisha utawala bora.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger