Mbunge
wa Ulanga, Godluck Mlinga (CCM) ameyatuhumu mashirika ya umma ambayo
hayajajiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwa watendaji
wake wakuu wamepewa malipo ya asilimia 10 ili mashirika hayo yajiunge na
kampuni binafsi za bima.
Ameyataja
baadhi ya mashirika hayo ya umma yaliyokaidi kujiunga na NHIF licha ya
kulazimishwa kisheria kuwa ni Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati
na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
“Yapo
mashirika ya umma yanakataa kujiunga na NHIF wakati sisi wabunge
tumejiunga, wao ni nani? Wakubwa wao wanapata asilimia 10 na wanajiunga
na kampuni za bima ya afya binafsi…
“Mimi
niliwahi kuwa Compliance Officer wa NHIF nikaenda TRA, nikawaeleza
umuhimu wa kujiunga NHIF unachangia pesa kidogo unapata huduma nyingi
lakini bosi wao akanijibu pesa si tatizo na afadhali ametumbuliwa huyo
bosi wao, yule angekuwa ofisini kwangu asingetoka,” alisema Mlinga na kuongeza:
“Kila
sehemu wananitaja Mlinga Mlinga, napata vitisho vingi lakini serikali
inanilinda na kama jeshi (JWTZ) limeweza kusambaratisha M23 itashindwa
kunilinda mimi…wengine wananiita teja hivi teja anavaa suti iliyonyooka
kama mimi, siwezi kukasirika kwa sababu si kweli lakini wangeniita
mbilikimo ningekasirika kwa sababu kweli.”
Mbunge huyo alitaka serikali ikomeshe tabia ya wanaume kubaka wazee na kufafanua “najiuliza wanawake wa mikoa yenye ubakaji wa wazee ni wagumu kuelewa hadi wazee wabakwe?”
Naye
Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby (CCM) amesema sasa ataanza kuacha
kuwashawishi wananchi wake kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
kutokana na mfuko huo kutopeleka dawa na chanjo za watoto kwenye vituo
vya afya, badala yake inapeleka kondomu na vifaa visivyo muhimu kwa
wananchi.
0 comments:
Post a Comment