Magari
ya washawasha jana yaliibua mjadala bungeni baada ya mbunge wa Viti
Maalumu, Susan Lyimo (Chadema) kubanwa athibitishe kauli yake aliyoitoa
kuwa serikali ilinunua magari ya Polisi ‘Washawasha” 777 wakati
ilitumia 50 pekee wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita.
Mbunge
huyo alitakiwa kuthibitisha hilo na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan
Zungu kwa kupeleka uthibitisho au kufuta kauli yake baada ya Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Massauni kuomba mwongozo
kupitia kanuni ya 64(a) na 63(1) akiomba mwongozo wa hatua gani anaweza
kuchukuliwa Lyimo.
“Kanuni
zipo, zinampa haki kila mbunge na Naibu Waziri ameomba mwongozo kwa
kanuni ya 64(a) na 63(1) sasa kwa kuwa Susan hayupo hapa sasa hivi,
akirejea jioni mwongozo wangu ni kwamba afute maneno yake au alete
uthibitisho,” alisema Mwenyekiti huyo wa Bunge.
Lyimo
katika mchango wake kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, alisema serikali imenunua magari ya ‘Washawasha” 777
mwaka jana wakati wa Uchaguzi Mkuu lakini yaliyotumika ni 50 pekee.
0 comments:
Post a Comment