Wanasema ukipenda boga, penda na maua yake.Kwa Diamond kumpenda Zari the Bosslady kunaamanisha kuyapenda pia
maua yake matatu ya mwanzo.
Unapompenda mwanamke ambaye tayari ana
watoto watatu kabla yako, ni lazima ukutane na changamoto nyingi hasa za
kutengeneza ukaribu na watoto hao. Wapo waliofanikiwa na wengi
wameshindwa. Kwa Diamond lakini ameonekana kuucheza vyema mchezo huu na
watu wamemsifia.
Jana ilikuwa ni birthday ya mtoto wa tatu wa Zari, Lil Q ambaye
katika wote anaonesha kumkubali zaidi Diamond kuliko wale wawili
wakubwa. Kuonesha kuwa anamkubali pia dogo huyo mkali wa kunyuka pamba,
Chibu alimtumia salamu za birthday kwenye Instagram zilizowavutia wengi.
“Happy Birthday to my Little Handsome… Mr Swag on point… i know he’s your Bae.. @lilQ_is_Bae,” aliandika.
“Happy Birthday to my Little Handsome… Mr Swag on point… i know he’s your Bae.. @lilQ_is_Bae,” aliandika.
Kwa post hizo, Diamond alichukua pointi zake tatu jana.
0 comments:
Post a Comment