Tuesday, May 3, 2016

Mama yake Tupac, Afeni Shakur Davis afariki dunia

Afeni Shakur Davis, mama yake hayati Tupac Shakur amefariki dunia. Alikuwa na umri wa miaka 69.

Mama huyo alipata mshtuko wa moyo Jana kabla ya kupelekwa hospitali alikopoteza maisha kabla ya saa nne na nusu usiku.

Shakur, aliyezaliwa kwa jina la Alice Faye Williams, alibadilisha jina lake baada ya kuhamia New York City na kujiunga na vugu vugu la Black Panther. 


Tupac aliwahi kumuimbia mama yake huyo kwenye wimbo ‘Dear Mama’ wa mwaka 1995 akielezea shida za utotoni na alivyomheshimu mama yake.

“There’s no way I can pay you back/But the plan is to show you that I understand/You are appreciated,” alirap Tupac.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger