Hospitali
ya Rufaa ya Amana, Ilala imewasimamisha kazi madaktari wawili na
muuguzi mmoja, kwa madai ya kumtolea lugha isiyostahili mjamzito Asha
Said (17), aliyejifungulia chooni.
Tukio
hilo lilitokea mwezi uliopita katika hospitali hiyo, baada ya Asha
kujifungulia chooni na madaktari na wauguzi hao kumtolea lugha chafu,
bila kuelezwa sababu za kufanya hivyo.
Mganga
Mkuu wa Amana, Dk Meshack Shimwela alisema jana kwamba watumishi hao
ambao hakuwataja wamepelekwa katika Baraza la Watumishi na Madaktari la
hospitali hiyo kwa uchunguzi zaidi.
“Kilichotokea siku ile ni kauli zilizotoka kwa watumishi hao kwenda kwa mama aliyejifungua, ambaye pia alikuwa mdogo kiumri.
“Sisi
madaktari na waaguzi tuna taratibu za kinidhamu, huwa tunazifuata baada
ya watumishi kubainika kufanya makosa, hatua ya kwanza ndiyo hiyo
tusubiri nyingine wakati uchunguzi ukiendelea dhidi yao,” alisema Dk Shimwela.
Dk
Shimwela ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania
(MAT), alisema kilichohitajika ni lugha nzuri kwa sababu kisheria ni
lazima kwa mgonjwa yeyote kuoga akifika hospitali, ili kumkinga na
maradhi mbalimbali.
Wakati
hayo yakitokea Amana, Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) kimeitaka jamii
kuendelea kuibua matukio ya unyanyasaji na huduma mbaya wanazofanyiwa
na wakunga wakati wa kujifungua, ili vyombo vinavyohusika viweze kuliona
tatizo kwa ukubwa wake na kulifanyia kazi.
Akizungumza
katika kongamano la siku mbili la kujadili maendeleo ya wakunga nchini,
rais wa chama hicho, Feddy Mwanga alisema kila wanaposikia malalamiko
kuhusiana na unyanyasaji na huduma mbaya kwa wajawazito, chama hicho
hufanya utafiti na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika.
0 comments:
Post a Comment