Kigogo
wa CCM aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Sukwa Said Sukwa amevishauri vyombo vya
dola visiwani Zanzibar kumchukuliwa hatua haraka Katibu Mkuu wa Chama
cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kwa kauli yake
aliyoihusisha na kosa la uhaini.
Sukwa
aliitaja kauli ya Maalim Seif aliyoitoa alipokuwa akihutubia katika
mkutano wa hadhara kisiwani Pemba kuwa Dk. Ali Mohamed Shein hatamaliza
kipindi chake cha urais mwaka 2020 na kwamba ni dikteta.
Sukwa amesema kuwa kauli hiyo ya Maalim Seif haipaswi kupuuzwa hata kidogo kwakuwa kauli kama hizo ni zaidi ya sumu.
“Sivilazimishi
vyombo vya dola kufanya ninavyotaka, lakini tunashauri tu visipuuze
ushauri wetu kwa sababu ulimi wa mtu unaweza kuwa sumu hatari kuliko
matendo yake,” Sukwa aliliambia gazeti la Raia Tanzania.
Maalim
Seif amekuwa akifanya mikutano kuwataka wananchi kumuunga mkono
kuikataa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Shein,
akieleza kuwa uchaguzi wa marudio haukuwa wa haki.
0 comments:
Post a Comment