Jeshi
la Polisi mkoani Mara linawashikilia wakazi wawili wa Mtaa wa Nyegezi,
Wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za kusafirisha dawa za
kulevya aina ya mirungi.
Kamanda
wa Polisi mkoani humo, Ramadhani Ng’anzi alisema jana kuwa watuhumiwa
hao walikamatwa Mei 17, saa nane mchana katika Kijiji cha Mulyaza
wilayani Butiama wakiwa na kilo 500 za dawa hizo zimehifadhiwa kwenye
vifurushi 15 yenye uzito wa zaidi ya nusu tani.
Alisema
watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha dawa hizo kwa kutumia gari aina
ya Toyota Carina lililokuwa likiendeshwa na mmoja wao wakitokea Sirari,
Wilaya ya Tarime wakielekea Mwanza.
Hata
hivyo, aliwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo
ili kusaidia kuwakamata watu wanaokiuka sheria na taratibu za nchi.
Baadhi
ya wakazi wa mjini hapa walisema udhibiti wa dawa za kulevya ni jukumu
la kila Mtanzania kwa sababu madhara yake husababisha athari katika
jamii inayozunguka eneo husika.
0 comments:
Post a Comment