Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata wasichana 15
katika nyumba iliyopo maeneo ya Ukonga, waliokuwa tayari kusafirishwa
kwenda Oman kufanya kazi za ndani.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi wa kanda
hiyo, Simon Sirro, alisema wasichana hao walikamatwa baada ya Polisi
kupata taarifa toka kwa msiri kuwa kuna mtu amewaweka wasichana kwa
ajili ya kuwasafirisha.
Sirro
alisema Polisi walifuatilia na kufika katika eneo hilo na kufanikiwa
kuwakuta katika nyumba ya Hadija Mohamed (40) wakiwa wamegawanywa katika
vyumba viwili.
Alisema
uchunguzi wa awali, umebaini kuwa mwanamke huyo anashirikiana na
mwenzake Salma Habibu (43) mkazi wa Temeke kuwatafutia masoko nchini
Oman na wao ni mawakala wanaoletewa kutoka mikoani na kuwapokea kwa
ajili ya kuwasafirisha.
Aidha alisema watuhumiwa hao watapelekwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Pia
ametoa onyo kwa watu wenye tabia hiyo kuacha, kwani wasichana hao
wakifikishwa nje ya nchi hufanyiwa vitendo vya kikatili na unyanyasaji.
Katika
tukio jingine, Polisi kanda hiyo imewakamata vijana 75, ikiwa ni
muendelezo wa msako wa vijana wanaofanya matukio ya wizi wa majumbani
nyakati za usiku.
0 comments:
Post a Comment