Mnamo
tarehe 11.05.2016 majira ya 13:30hrs mchana katika barabara ya Mwanza –
Simiyu eneo la Igoma Kata ya Nyakato Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa
Mwanza, gari namba T. 488 CDZ aina ya Scania Tractor likiendeshwa na
dereva aitwaye Enock Mshihiri miaka 24, msukuma mkazi wa Igoma
lilimgonga mwendesha baiskeli aitwaye Sanyiwa Nengo miaka 60, msukuma
mkazi wa Busekwa na kusababisha kifo chake papo hapo.
Chanzo
cha ajali ni uzembe wa dereva wa Scania kushindwa kulimudu gari
alipokua barabarani. Mtuhumiwa wa ajali hiyo amekamatwa, pindi uchunguzi
ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayo mkabili.
Mwili wa marehemu upo hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya
uchunguzi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi AHMED
Z. MSANGI anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya
moto ikiwa nipamoja na kufuata na kuheshimu sheria na alama za usalama
barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Lakini
pia anatoa wito kwa watumiaji wengine wa barabara wakiwemo watembea kwa
miguu nao wachukue tahadhari pindi wanapokua barabarani.
Imetolewa na:
SACP. AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
0 comments:
Post a Comment