Kwamba
tarehe 11.05.2016 siku ya jumatano majira ya saa 03:45hrs usiku katika
Kijiji na Kata ya Sima Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, watu wawili
wasiofahamika majina wakiwa na mapanga walivunja mlango na kuingia
kwenye nyumba ya Mama Eugenia Philipo miaka 60, akiwa amelala na familia
yake na kuwakata mapanga sehemu mbalimbali za miili yao hadi kufariki
papo hapo, Mama mwenye Kaya Bi Eugeni, Mdogo wake, Watoto, pamoja na
watu wengine wawili waliokua wakifanya kazi hapo nyumbani kwao wakitokea
Ngara Mkoani Kagera.
Waliouawa
1. Eugenia Philipo miaka 60 Mama mwenye Kaya, 2. Maria Philipo miaka
50, mdogo wa Mama Mwenye Kaya 3.Mabula Makeleja miaka 20 mwanafunzi wa
kidato cha nne, 4. Mkiwa Philipo mika 12, mwanafunzi shule ya msingi 5.
Leonard Aloyce miaka 13 mwanafunzi shule ya msingi sima wote wa familia
moja na 6. Donald miaka 40, pamoja na 7. Samson miaka 23 wakazi wa Ngara
waliokuwa wakifanyakazi hapo nyumbani kwa Bi Eugeni.
Aidha
katika utekelezaji wa mauaji hayo watu hao walianza kuingia kwenye
nyumba walipokuwa wamelala watoto wa familia hiyo pamoja na wafanyakazi,
na baada ya kuwakata mapanga hadi kuwaua waliingia kwenye nyumba ya
jirani alipokuwa amelala Mama mwenye Kaya na mdogo wake Bi Maria na
kuwaua vivyo hivyo, kisha wakaondoka eneo la tukio na kwenda kusiko
julikana. Huku watoto wengine wanne wakinusurika kwenye mauaji hayo
baada ya kujificha chini ya uvungu wa kitanda.
Jeshi
la Polisi linawashikilia watu nane kwa mahojiano dhidi ya mauaji hayo
na msako mkali wa kuwasaka wahusika wengine waliohusika kwa namna yeyote
katika mauaji hayo bado unaendelea.
Chanzo
cha mauaji hayo bado hakijajulikana, uchunguzi bado unaendelea. Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mwanza linawaomba wananchi wenye mapenzi mema na nchi
yao watusaidie kutupa taarifa za wahusika wa mauaji hayo ili tuweze
kuwakamata.
Imetolewa na:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
0 comments:
Post a Comment