Tuesday, May 10, 2016

Chadema: Bunge la Sasa Kibogoyo Limeng'olewa Meno na Serikali

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk Vincent Mashinji amesema kitendo cha Serikali ya Awamu ya Tano kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge ni sawa na kuling’oa meno bunge hilo.

Tofauti na mikutano miwili iliyopita ya Novemba 2015 na Januari/ Februari 2016, Serikali hii inayoongozwa na Rais John Magufuli, iliamua kufuta matangazo ya moja kwa moja ya Bunge la Bajeti lililoanza vikao vyake Aprili 19 kwa maelezo kwamba ni gharama kubwa kwa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC). Badala yake TBC huonyesha kipindi cha maswali na majibu pekee na hurekodi matangazo mengine na kurushwa katika kipindi cha ‘Leo katika Bunge’ saa nne usiku.

Suala hilo lilipingwa vikali na wabunge wa upinzani lakini uongozi wa Bunge ulitia chumvi kwenye kidonda baada ya kukataza vyombo vya habari kupiga picha za video, badala yake wanatakiwa kuchukua picha kutoka kwa televisheni ya Bunge.

Akizungumzia hali hiyo jana jijini Dar es Salaam, Dk Mashinji alisema kuwa huu ni mkakati maalum uliosukwa na CCM ili kuvibana vyama vya upinzani.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger