Kiongozi Mkuuwa Chama cha
Allience for Change and Transparency(ACT), Zitto Zuberi Kabwe, ameibuka
na kujibu mashambulizi juu ya taarifa zinazoenezwa na Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kupitia Umoja wa Vijana wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) za kumhujumu Rais Dk. Magufuli katika utendaji wake.
Kiongozi huyo amesema anaushahidi wa moja kwa moja juu ya vitendo vinavyofanywa na Waziri huyo katika kueneza propaganda zinazolenga kuiyumbisha Serikali .
“Nina
ushahidi usio na mashaka wa Kitwanga kupanga Vijana wanaojiita wa UVCCM
kufanya mikutano na Waandishi wa Habari na anawalipa fedha kufanya
hivyo, nataka ieleweke wazi kuwa nina muunga mkono Rais katika kazi ya
kusafisha Nchi … nitakuwa mtu wa ajabu nisipo muunga mkono katika vita
dhidi ya ufisadi” amesema Zitto Kabwe.
Zitto
amemtaka Waziri Kitwanga kuepuka siasa za porojo na kusema waziri huyo
si ‘size’ yake na hana mpango wa kumtoa katika nafasi ya uwaziri hivyo
aache kulalamika na kueneza uzushi.
“Kimsingi
nashangaa mtu kama yeye (Kitwanga) kuweza hata kuwa Waziri wa Wizara
nyeti kama hiyo, zaidi ya yote Waziri Kitwanga sio ‘size yangu’.
Naanzaje kuhangaika na Kitwanga? Ili iweje? Namsihi asijipandishe chati
kwamba mimi nataka kumtoa (uwaziri) . Ningetaka kumtoa wala asingejua
maana ningeshughulika na aliyemteua”Amesisitiza Kabwe.
Hata
hivyo Kabwe amemtaka Waziri Kitwanga kujipima kama bado anastahili
kuendelea kukaa katika nafasi yake ya uwaziri kutokana na kashfa ya
kampuni anayo imiliki iitwayo Infosys kwa kushirikiana na Kampuni ya Lugumi kuiingizia
Serikali hasara ya shilingi bilioni 34 kupitia Zabuni ya kununua vifaa
vya kutekeleza mradi wa utambuzi wa vidole kwenye Vituo vya Polisi
nchini.
“Nawasihi
Watanzania wote kumdharau Waziri Kitwanga nakumtaka ajibu tuhuma
zinazomkabili za kampuni yake binafsi kufanya kazi na Idara katika
Wizara anayosimamia na kwamba ajipime kama anatosha kuendelea kumsaidia
Rais kazi.” Aliongeza Kabwe.

0 comments:
Post a Comment