Thursday, April 28, 2016

Urusi Kuwekeza Hapa Nchini

 
Tanzania imewapokea wafanyabiashara 50 kutoka Urusi kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali nchini.

Akieleza ujio wa wafanyabiashara hao, Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Adolf Mkenda alisema baada ya kushirikiana kisiasa kwa muda mrefu, Urusi imeamua kuisaidia Tanzania kuimarisha uchumi wake.

Wafanyabiashara hao wanatarajia kukutana leo katika kongamano litakalobainisha fursa zilizopo kwa wageni hao kuwekeza hasa kwenye kilimo, nishati, usafiri, viwanda na madini.

Urusi ni miongoni mwa mataifa 10 makubwa kiuchumi duniani na imeendelea kisayansi na kiteknolojia huku ikiwa na idadi kubwa ya watu.

Rais mstaafu, Jakaya Kikwete wakati akiwaaga mabalozi 36 wa Tanzania, aliwaagiza kulitangaza Taifa huko waliko ili kuvutia wawekezaji na kuwaongezea masoko Watanzania.

Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Wynjones Kisamba ameanza kuonyesha njia kwa ugeni huo unaotarajia kuongeza biashara za Taifa hilo.

Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Julieth Kairuki alisema Watanzania wana uhakika na soko la mbogamboga, matunda, asali na bidhaa nyingine nchini humo na kwamba kinachotakiwa ni kuongeza ubora ili kukidhi viwango vya kimataifa.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger