TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Afisa mtendaji huyo aliomba pesa hiyo ili aweze kumpatia dhamana ndugu wa bwana JOHN MASHOMALI LUKUNGU(45), Bi LUCIA SOBOLA JANELA ambaye yeye kama mlezi alikamatwa kwa kosa la utoro wa mwanafunzi LUCIA MABULA JOHN.
Mtuhumiwa BW. BONAVENTURA LUPILYA MAKUNGU alitenda kosa hilo la kuomba na kupokea hongo mnamo tarehe 26/02/2016 ambapo ni kinyume na kifungu cha 15(1a) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11/2007.
Mashtaka hayo yamefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kwimba na Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Bw. JOVINE MAJURA ambapo yamesajiliwa kwa shauri la jinai namba 39/2016 na liko mbele ya Mheshimiwa Hakimu BONAVENTURA LEMA.
Akisomewa shauri hilo mbele ya Hakimu, Mtuhumiwa BW. BONAVENTURA LUPILYA MAKUNGU(46) alikana shtaka hilo na yuko nje kwa dhamana hadi shauri hilo litakapotajwa tena tarehe 24 Mei, 2016.
Wakati huohuo TAKUKURU Mkoa wa Mwanza pia inatarajia kumfikisha mahakamani Afisa Afya na Mazingira Bw. SOSPETER JACOB SELEWA (29) wa kata ya Buswelu iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, kwa kosa la kuomba rushwa ya shilingi Laki 100,000/= kutoka kwa Bi. LYDIA JULIUS TAMBILIJA ambaye ni mmiliki wa kituo cha kulelea watoto kinachofahamika kwa jina la JITAMBUE.
Afisa Afya huyo aliomba pesa hiyo ili aweze kufungua kituo hicho cha kulelea watoto ambacho awali alikifunga kwa vile kituo hicho hakikuwa na baadhi ya sifa zinazostahili.
0 comments:
Post a Comment