Baada ya wimbo wa ‘Freedom’ kufanya vizuri kwenye media mbalimbali, Sugu
anajipanga kuandaa shindano litakaloshindanisha nyimbo itakayoizidi
wimbo huo.
Siku kadhaa zilizopita baada ya Sugu kuachia video ya wimbo wa
‘Freedom’ ulizua taharuki baada Mr Blue kulalamika kuwa Sugu kamuibia
wimbo wake kabla ya uongozi wa studio ya MJ Record ambapo wimbo huo
ulitayarishwa kuliweka sawa tatizo hilo.
Akizungumza kwenye kipindi cha FNL, kinachoruka kupitia EATV, Sugu
amesema ‘tutaandaa shindalo la kushindanisha nyimbo itakayoizidi wimbo
wa ‘Freedom’.
“Tumeshaongea na media moja ambayo tutapeleka wimbo wa ‘Freedom’ ambao
wasanii wanaotaka watarekodi wimbo wataupeleka hapo. Kutakuwa na majaji
kwenye shindano hilo watakao chagua nyimbo kumi bora na baadae kupata
nyimbo moja. Mshindi kwenye shindano hilo atapata shilingi milioni
tano,” aliongezea.
Sugu amesema kwenye shindano hilo halitabagua msanii yeyote kila mtu anaruhusiwa hata awe Mr Blue.
0 comments:
Post a Comment