Mkurugenzi
wa Jiji la Dar es Salaam aliyesimamishwa kazi, Wilson Kabwe amesema
hahusiki na tuhuma zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda.
Kabwe
alitoa kauli hiyo, baada ya kutafutwa na mwandishi wetu ili kupata
maoni yake baada ya Rais Dk. John Magufuli kutangaza kumsimamisha kazi.
Mwandishi: Habari mkurugenzi?
Kabwe: Salama.
Mwandishi: Tumepata
taarifa za kusimamishwa kwako kazi na Rais kutokana na tuhuma
zilizotolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda tunaomba
maoni yako.
Kabwe: Sijasikia ndiyo kwanza unaniambia wewe, kasema lini Rais?
Mwandishi:Leo wakati akizindua Daraja la Kigamboni.
Kabwe: Alitamka palepale au?
Mwandishi: Ndiyo.Nataka kujua unazungumziaje uamuzi huo?
Kabwe alisema tuhuma zinazoelekezwa kwake ni za uongo na kwamba zimelenga kumchafua mbele ya Rais Magufuli.
Mkurugenzi
huyo alishangaa kuhusishwa na tuhuma hizo na kusema kuwa, wakati sheria
ndogo zinapitishwa na uongozi wa Jiji la Da es salaam yeye hakuwa
Mkurugenzi wa Jiji hilo.
“Sihusiki na mikataba inayosemwa, huu ni uongo mtupu, Makonda ametoa taarifa za uongo kwa Rais.
“Tuhuma
zinazoelekezwa kwangu ni za uongo na zimelenga kunichafua mbele ya
Rais, nasisitiza tena hakuna mkataba wowote ambao ofisi yangu iliingia
kwa nia ya kupoteza mapato ya Serikali,” alisema Kabwe huku akihoji kuwa ikibainika hahusiki atalipwa fidia?
KUHUSU KUSTAAFU KAZI
Alisema
kutokana na hali ya afya kutokuwa nzuri, Desemba mwaka jana aliomba
kustaafu utumishi wa umma na kuandika barua kwa Rais ili aendelee na
matibabu.
Alisema
tangu aandike barua hiyo, hajawahi kujibiwa na kusisitiza kuwa
anamheshimu Rais Magufuli na anaamini atatenda haki baada ya vyombo
husika kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo.

0 comments:
Post a Comment