BOSI wa kundi la Cash Money, Bryan Williams ‘Birdman’, amewajia juu watu ambao wanalidharau kundi hilo na kulitia ubaya.
Kuna baadhi ya mashabiki walikuwa wanalisema vibaya kundi hilo kwamba
bosi huyo anawanyanyasa wasanii wake na kusababisha wengine kulikimbia
kundi hilo.
Kutokana na hali hiyo, msanii huyo amewataka wadau na mashabiki wa
muziki kuliheshimu kundi na kudai kwamba wao hawana mchango wowote hadi
hapo lilipofika.
“Nashangaa kuona baadhi ya watu wakishambulia Cash Money, hii haina
maana yoyote kikubwa ni kuheshimu kazi za watu kila mmoja ana mambo yake
ya kufanya hivyo sioni sababu ya kulizungumzia kundi na jina langu.
“Wasanii ambao wapo kwenye kundi wanafanya vizuri na wanaridhika na
kile ambacho kinaendelea na ndio maana baadhi yao wapo,” alisema
Birdman.
0 comments:
Post a Comment