Basil Mramba na Daniel Yona wakiwa Mahakama Kuu ya Tanzania kusikiliza rufaa yao.
Daniel Yona akiteta jambo na mmoja wa mawakili mahakamani hapo.
Yona akiwasiliana na ndugu zake.
MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam leo imetoa hukumu ya rufaa dhidi ya mawaziri wa zamani, Bazil Mramba na Daniel Yona waliohukumiwa kifungo cha miaka mitatu na faini ya milioni tano baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Projest Rugazia ametupilia mbali rufaa yao ila wamepunguziwa adhabu kutoka miaka mtatu hadi miwili na kwa sasa hawatalipa faini.
Mapema Agosti 5, mwaka huu mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Rugazia iliagiza pande zote mbili kuwasilisha hoja za kusikiliza rufaa hizo kwa njia ya maandishi.
Upande wa Jamhuri ulikata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumwachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja, kwamba ushahidi uliotolewa haukuthibitisha makosa dhidi ya tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.
Kadhalika, Mramba na Yona walikata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yao ya kifungo cha miaka mitatu na faini ya milioni tano
0 comments:
Post a Comment