Tuesday, October 6, 2015

Video: Serikali YAKANUSHA Kifo cha Mhe. Abdallah Kigoda


Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali inapenda kukanusha taarifa kutoka Kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda na Biashara amefariki dunia nchini India alikokuwa anatibiwa.

Taarifa Rasmi ya serikali kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata Chembe ya ukweli. Mhe. Dkt. Kigoda bado yupo nchini India Katika Hospitali ya Apollo katika Jiji la New Delhi anakoendelea kupatiwa matibabu.

Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015 na tangu kipindi hicho amendeleza kupata matibabu katika hospitali Hiyo ya Apollo.

Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa serikali.

Imetolewa na Assah Mwambene,
Msemaji Mkuu wa serikali
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger