Mmoja wa majeruhi katika shambulio la Oregon akipatiwa huduma ya kwanza.
Muuaji wa watu tisa katika shambulio hilo, Chris Harper-Mercer, 26, enzi za uhai wake.

Baadhi ya wafanyakazi na wanafunzi wa Umpqua wakiwa na sintofahamu baada ya kutokea shambulio hilo.
Waombolezaji wakiwa na simanzi baada ya shambulio la jana.
Wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo cha Umpqua jimboni Oregon nchini Marekani wakikaguliwa wakati wakitoka chuoni hapo.
WATU tisa wameuawa na wengine saba
kujeruhiwa baada ya kijana mmoja kushambulia kwa risasi katika Chuo
kimoja kilichopo Roseburg jimboni Oregon, Marekani jana.
Kijana huyo aitwaye Chris Harper-Mercer, 26, akiwa na silaha
alifyatua risasi kwenye Chuo cha Umpqua na kuua watu tisa kisha na yeye
kuuawa wakati alipokuwa akijibizana kwa risasi na polisi.Sababu za muuaji huyo kutekeleza shambulio hilo bado hazijajulikana, ingawa polisi wanasema wanafanyia uchunguzi ripoti kuwa alitahadharisha dhamira yake hiyo katika mtandao wa kijamii.
Saa kadhaa baada ya shambulio hilo, ambalo watu saba walijeruhiwa, Rais wa Marekani, Barack Obama ametaka kuwe na sheria kali za udhibiti wa silaha.
0 comments:
Post a Comment