Siku chache baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kutoa tamko la kuufungia wimbo wa Roma ‘Viva’, rapa huyo amesema kuwa bado hajapata barua rasmi ya Baraza hilo.
Amesema yeye pia ameiona habari hiyo kwenye mitandao na sababu zilizoainishwa na Baraza hilo kuifungia ‘Viva’.
Licha ya kukiri kuwa hafahamu taratibu zinazotumiwa na Baraza hilo kutoa taarifa kama hizo, Roma alilishauri Baraza hilo kuweka utaratibu wa kuzisikiliza nyimbo kabla hazijatoka ili kuepusha usumbufu.
"Nisiwe muongo, sijui taratibu wanazotumia kufikisha taarifa zao.Mi nadhani ingekuwa rahisi kama artist hajaachia nyimbo yake mpya ama hajafanya kazi yake ya sanaa,iwe inawasilishwa katika hicho chombo.Nadhani hapo tungekuwa tunaenda sawa," amesema Roma.
Hata hivyo,Afisa habari wa BASATA,Artistide Kwizela amefafanua taratibu zinazotumiwa na baraza hilo kufikisha ujumbe kwa umma pale wanapoifungia kazi fulani ya msanii.
"Kuna kufungiwa kwa maana ya msanii mwenyewe kuandikiwa,lakini kama kuna taarifa imetoka public kwamba nyimbo za namna hiyo zimezuiliwa, kuna two ways.....Either barua kuandikwa kwa msanii au Public anouncement kwamba wimbo fulan umefungiwa"
0 comments:
Post a Comment