Wednesday, September 30, 2015

Airtel yatoa gawio la Tshs Bilioni 5.3 kwa wateja wa Airtel Money‏

Meneja biashara wa kitengo cha Airtel Money, Bwn Asupya Naligingwa (kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza Airtel kugawa gawio la faida la zaidi ya shilingi billion 5 kwa wateja na mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel Money nchi nzima. Pichani ni Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania Bi Jane Matinde.

Dar es Salaam, Jumatano 30 Septemba 2015, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza kugawa zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa wateja na mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel Money nchi nzima Uamuzi huo wa kutoa gawio la faida lililopo katika akaunti ya udhamini ya wateja wa Airtel Money (Trust account) litawawezesha wateja wa Airtel kulipwa kiwango kizuri cha gawio la faida.

Kiwango hiki cha pesa kitalipwa kutokana na kiasi cha pesa mteja alichokuwa nacho kwenye akaunti yake ya Airtel Money kila mwisho wa siku kuanzia March 2014 hadi April 2015.
Akiongea na waandishi wa habari,Meneja wa kitengo cha Airtel Money, Asupya Nalingigwa, alisema wanayo furaha kutangaza mgawanyo huu wa gawio la faida kwa wateja wao baada ya benki kuu ya Tanzania. Kuidhinisha kutoa pesa hizi katika akaunti ya udhamini ya pesa za wateja wa Airtel Money ijulikanayo kama trust account.

Aliongeza kwa kusema wateja wa Airtel Money watapata sehemu ya gawio lao kulingana na salio wanalokuwa nalo kwenye akaunti zao kila siku”Tunaamini kiasi hiki cha pesa kitachangia kwa kiasi kikubwa katikakuboresha maisha ya watanzania wengi , kuwahamasisha wateja wasiofikiwa na huduma za kibenki kutumia mfumowa pesa kwa njia ya simu.

Vilevile wateja wetu wa Airtel Money wataendelea kutumia huduma za pesa kupitia simu za mkononi, kufanya miamala yao ya kila siku na kutunza pesa zao ili kupata gawio lao kila watakapo weka pesa katika akaunti zao za Airtel Money”. Aliongeza Nalingigwa Uamuzi huu wa kutoa gawio la faida kwa wateja ni wakuungwa mkono kwani unachochea na kuboresha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu za mkononi , ukizingatia takribani asilimia 85% ya watanzania bado hawajafikia na huduma za kibenki
Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma za kibunifu za kifedha kupitia simu za mkononi ikwemo NFC huduma inayokuwezesha kufanya malipo kupitia kadi, Mikopo ya Timiza na huduma nyingine nyingi.

Katika maelezo yake Naligingwa aliahidi Airtel kuendelea na dhamira yake ya kuzindua huduma bora na za kisasa katika mienzi ijayo ili kuwanufaisha watanzania waishio maeneo ya mijini na vijijini
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger