Saturday, July 18, 2015

Sheikh mkuu awaonya mastaa wa filamu na muziki


ONYO! Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim amewaonya mastaa wa filamu na muziki nchini kutorudia dhambi ambazo wamefutiwa kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, sheikh huyo alisema kuwa mwezi huo ni wa kujisafisha na  watu wengi hufanya ibada na kuacha yale yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu hivyo iwapo wasanii waliosafishwa wataamua kurudi kwenye dhambi ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

Mbali na mastaa sheikh huyo amewafungukia watu wote lakini aliwasisitizia mastaa kwa sababu wengi wao mwezi mtukufu wa Ramadhani huachana na mambo mengi ikiwa ni pamoja na mavazi ya hasarahasara hivyo ni vyema wakajirekebisha.

Nawaonya hata kwa mavazi yao, ilikuwa ikipendeza kuwaona wakijistiri lakini kama watarudia mavazi hayo na matendo mabaya ya kuwasababishia dhambi basi mwezi mtukufu hautakuwa na maana kwao,” alisema sheikh.

Mastaa wengi mwezi wa Ramadhani walionekana kwenye nyumba za ibada na wanawake wengi walikuwa wakijistiri huku wakitoa misaada mbalimbali na kufuturisha pia lakini kumekuwa na kasumba ya kurudia maovu saa chache baada ya kumaliza mfungo.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger