Tuesday, July 21, 2015

Picha: Mlipuko wa bomu waua 27 na kujeruhi 100 Uturuki

Mmoja wa majeruhi katika mlipuko huo.
Hali ilivyokuwa baada ya mlipuko kutokea.
Majeruhi akipatiwa huduma ya kwanza.
TAKRIBANI watu 27 wameuawa huku wengine 100 wakijeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga lililotokea leo katika Mji wa Suruc nchini Uturuki.
Mji huo wa Suruc upo kwenye mpaka wa Uturuki na nchi ya Syria.
Mlipuko huo ulitokea kwenye bustani ya kituo cha kitamaduni leo huku mamia ya vijana wakiripotiwa kufanya kazi kwenye kituo hicho.
Mji wa Suruc, unapakana na mji wa Syria wa Kobane, ambao unawahifadhi wakimbizi wengi waliokimbia mapigano katika miezi ya hivi karibuni.
CREDIT: BBC
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger