Sunday, July 19, 2015

Picha: Mama Salma Kikwete ahudhuria mazishi ya Banza Stone

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akilakiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrer Mngereza alipowasili kujiunga na familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam  Jumamosi Julai 18, 2015. Marehemu Banza Stone, aliyefariki jana mchana baada ya kuugua kwa muda mrefu,  amezikwa jioni hii katika makaburi ya Sinza. Marehemu Banza Stone atakumbukwa kwa umahiri wake wa utunzi na uimbaji alipokuwa na bendi mbalimbali zikiwemo Twanga Pepeta, Tot na Extra Bongo.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika  alipowasili kujiunga na familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam 
 
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji Haji Ramadhani Masanja, mtoto wa marehemu   katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam
 Waombolezaji wakilia kwa uchungu wakati mwili wa Banza Stone ukipelekwa mazikoni
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger