Monday, July 20, 2015

Mume apigwa kila siku na mkewe na kudhalilishwa hadi kutemewa mate mbele ya watoto,kisa hana kazi


Mwanaume wa miaka 35 huko Ashanti,ghana aomba msaada kutokana na mateso anayopewa na mke wake.

Kwa mujibu wa Abrafi Owusu,mke wake alibadilika kuwa 'monster' baada ya yeye kupoteza kazi kwenye kampuni aliyokuwa anafanya kazi.

Baba huyo wa watoto wawili amefichua mambo hayo alipokuwa kwenye interview na redio moja wapo nchini umo,alisema kwamba anakabiliwa na vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa mke wake kwa sababu ya maudhi madogo madogo tu.

"Kwasababu siwezi kutimiza wajibu wangu kama baba,mke wangu ananitreat mimi kama tambala chafu na ananipiga makofi anapojisikia kama majibu yangu yamemuudhi."

Kuongezea chumvi kwenye kidonda Mr Owusu anasema kuwa mke wake huyo anamnyima 'unyumba' wanapokua katika hali yao ya kawaida hasa usiku.

"Siku hizi ananitemea mate mbele ya watoto wetu, ananiambia me sio wa 'level' yake kwasababu sina kazi, mume huyo aliongea na Nhyira FM huku machozi yanamtoka.

Mr Owusu sasa anatafuta talaka aokoe maisha yake kutoka kwenye unyanyasaji wa mara kwa mara na udhalilishaji kutoka kwa mkewe. 
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger