Monday, July 20, 2015

Inasikitisha...Mchepuko wa mchezaji maarufu wa zamani amteka mke wake na kumuua,kisha na yeye ajipiga risasi

Mchepuko wa mchezaji wa zamani wa NFL Buster Barnett, aliyejulikana kwa jina la Lisa Brown,49,(kwenye picha juu kulia) alimteka na kumuua mke wake Sadra Barnett,58 (kwenye picha chini). Alhamis iliyopita alimuua mke wa mchezaji huyo baada ya kukimbizana sana na polisi  na kushindwa alafu akajipiga risasi na yeye.

Kutokana na taarifa tulizopata, Buster 56,alikua anamahusiano ya kimapenzi na Lisa kwa miaka mingi sana na alimuahidi kumuoa. Siku hiyo ya tukio,jumatano asubuhi, Buster aliwaambia polisi kuwa Lisa alikuja kazini kwake baada ya kujua kuwa anaenda likizo na mke wake. Alithibitisha uwepo wa safari hiyo kwa Lisa ambaye aliondoka kwa hasira. Buster  akasema hakuwahi kufikiria kama Lisa anaweza kufanya kitu kama hicho kwahiyo hakutoa taarifa polisi.
Lisa na hasira zake akaondoka kazini kwa Barnett akaelekea nyumbani kwake Ellenwood ambako Sandra alikua peke yake.Lisa alipofika nyumbani hapo, Sandra alikua anaongea na simu na rafiki yake . Rafiki huyo wa Sandra alisema alisikia kama kuna vurugu  alafu Sandra alikua anasema ' Please dont hurt me' kabla simu haijakatwa kwahiyo haraka haraka akamwambia rafiki yake mwingine aende akamcheck Sandra.
By the time huyo aliyeagizwa anafika nyumbani,gari la Sandra lilikua limepaki tu kwahiyo akahisi hakuna tatizo. Kumbe muda huo,Lisa alikua ashamteka Sandra kwenye gari yake aina ya SUV- Dodge Durango inayomilikiwa na Buster.
Majirani walitoa taarifa polisi baada kuona jirani yao anagombana kwenye gereji yake na mtu ambaye aliwaletea mashaka na baada ya muda wawili hao walionekana wakiondoka kwenye SUV.
Polisi wa kata hiyo ya Carroll waliiona gari iliyoripotiwa alhamis na kuanza kukimbizana nayo mpaka Alabama. State Patrol  troopers wa Alabama nao wakajiunga kumkimbiza baada ya kukimbizana huko kuvuka mipaka ya nchi. Ghafla Durango ikasimama katikati ya Barabara. Polisi wanasema muda huo Lisa alimpiga Sandra risasi alafu na yeye akajipiga risasi.
Utekaji huo unaonyesha kuwa ni wa kudhamilia kwasababu polisi wamekuta vitu kama pingu na baadhi ya risiti. Buster hatuhumiwi kwa uhalifu wowote uliotokea au kupanga njama na Lisa kumuua mke wake.
Inasemekana kuwa sio mara ya kwanza kwa Lisa kumteka mtu,kwasababu alikua bado on probation kwa kosa la kumteka mtoto wake mwaka 2013,after losing custody.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger