Wednesday, November 6, 2013

Ajali ya pikipiki yaua wawili jijini Mwanza....Tunaomba radhi kwa picha.

Watu wawili wamefariki dunia papo hapo wilayani Bukombe mkoani Geita wakitumia usafiri wa bodaboda kufuatia pikipiki waliyokuwa wakisafiria kuteleza kwenye mchanga ikiwa kwenye mwendo kasi na kisha kukanyagwa vibaya vichwani na gari aina ya Noah ambayo walikuwa wakipishana nayo.
 
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo,  dereva wa bodaboda ambaye alikuwa na abiria wake mwanamke mwenye mizigo, alikuwa katika mwendo wa kasi. 

Hatua kadhaa kabla ya kupishana na gari hilo, matairi ya pikipiki yake yalishindwa kuhimili mchanga uliopo barabarani ndipo alipokosa uwiano wa kumiliki chombo hicho cha usafiri na kutereza kisha wakaanguka katikati ya barabara.
 
Sekunde chache gari la abiria aina ya Noah ambalo mpaka shuhuda huyo anaondoka kwenye tukio la ajali hakufanikiwa kulinasa namba zake likiwa kwenye kasi liliwapitia vichwani bodaboda na abiria wake ambao walikufa papo hapo.
 

-Gsengo.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

1 comment:

  1. inasikitisha sana inabidi hatua za haraka kuchukuliwa maana boda boda zimekuwa chanzo cha ajali nyingi sana hapa nchini,poleni sana waliopoteza wapendwa wao,mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi AMEEN

    ReplyDelete

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger