Friday, April 5, 2013

MFANYABIASHARA ALIYEUAWA CHINA NA MAITI YAKE KUKAA MONCHWARI MWAKA MZIMA AZIKWA JIJINI MWANZA...!!





MFANYABIASHARA, Mkumbukwa John Shayo (37)  (pichani) aliyefariki katika kifo chenye utata nchini China amezikwa Jumatano iliyopita na kulifanya Jiji la Mwanza kutawaliwa na majonzi.
Umati wa watu ulihudhuria mazishi hayo nyumbani kwa bibi wa marehemu, Mabatini kisha kuelekea katika Makaburi ya Buzuruga, Nyakato na kila mtu alionekana kujawa na huzuni.
Hata hivyo, mazishi hayo yaliathiriwa kidogo na mvua iliyofanya baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki washindwe kuuaga mwili wa marehemu.
Mkumbukwa alifariki China na maiti yake kuhifadhiwa hospitali kwa takriban mwaka mzima na serikali ya nchi hiyo huku mkewe, Neema Majukano pamoja na rafiki wa marehemu aitwaye Haji Msongore wakilaumiwa kwa kushindwa kutoa taarifa mapema juu ya kifo hicho.
Aidha, utata umegubika kifo cha Mkumbukwa kufuatia rafiki huyo wa marehemu ambaye mara ya mwisho walikwenda wote nchini Chini kudaiwa kumuoa mke wa marehemu, Neema.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger