Diamond akiwa mbele ya Prado yake siku alipoamua kuitangaza kwenye media june 2012.
Tofauti na Prado aliyoinunua june 2012, Diamond hajataka kutaja ni aina gani ya gari aliloliagiza sasa hivi lakini kakubali kwamba kaliagiza Japan na litakua la gharama ya juu kuliko Prado.
Ukiachia mbali hilo gari analoliagiza, Diamond amekiri pia kwamba amemaliza kuijenga nyumba yenye gharama ya milioni mia mbili sitini ambayo ameijenga maalum kwa ajili ya mama yake mzazi.
Diamond ambae amekua akiandamwa na maneno maneno ambayo anaamini wanaoyasambaza ni wasiompenda amesema “mimi nikimtanguliza Mwenyenzi Mungu mbele ata mtu atake kunifanya kitu gani haweziii mpaka aandike Mwenyenzi Mungu mwenyewe, ndio maana wao kila wakipiga vita… mimi nazidi kuwa maarufu, nazidi kuwa na hela… sasa hivi nabadilisha Prado nanunua gari jingine….. jamani mtaiona”
Unaweza kumsikiliza mwenyewe akiongea hapa chini.
0 comments:
Post a Comment