KICHENI pati ya mcheza filamu mkali Bongo, Aunt Ezekiel (pichani) iliingia dosari baada ya bibi wa staa huyo kutinga ndani kwenye kiti cha magurudumu kwa ajili ya wagonjwa (wheel chair) akitokea Hospitali ya Ocean Road ambako amelazwa kwa matibabu.
Ishu hiyo ilijiri Oktoba 24, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar ambako shughuli hiyo ilikuwa ikifanyika.
Aunt baada ya kumwona bibi yake huyo akimsogelea huku akisukumwa kwenye kiti cha magurudumu, aliumia na kuanza kumwaga machozi bila kujali shughuli yake.
Achilia mbali Aunt, ndugu wengine wakiwemo marafiki wa Aunt nao walilazimika kulia kwani kitendo cha bibi huyo kuacha kitanda huku anaumwa na kutinga ukumbini kilionesha ni jinsi gani alivyompenda mjukuu wake huyo.
Hata hivyo, bibi huyo alimsihi mjukuu wake anyamaze ili asherehekee siku yake hiyo kwa amani kwani amefurahi kujumuika naye lakini cha ajabu na yeye alianza kulia.
Baada ya picha ya vilio na majonzi tele, mambo yaliendelea kama ‘kawa’ ukumbini hapo.
Mastaa waliofungua shampeni siku hiyo ni Yvonne Sheryl Ngatikwa ‘Mona’, Lilian Intaneti, Illuminatha Poshi ‘Dotnata’ na Aunt Ezekiel mwenyewe.
Sherehe kubwa ya kuagwa Aunt inafanyika leo kwenye Hoteli ya Serena, jijini Dar huku sherehe ya harusi ikitarajiwa kufanyika Dubai mwezi ujao.

0 comments:
Post a Comment