Friday, October 26, 2012

MWISILAMU KAKOJOLEA KORAN NA KUMVISHA MBWA TASIBILI HUKO PEMBA !!!

Wakati sakata la kijana wa Mbagala kukojolea kitabu kitakatifu likiwa
bado bichi mahakamani.
Huko Pemba maeneo ya Chakechake kijiji cha Wawi mwislamu amekashifu kitabu
hicho kwa kukikojolea  kumvisha mbwa tasibii na kumlazimisha mama yake
kumpakata mbwa huyo.

Mtu huyo mwanamme baada ya kutenda tukio hilo kajipeleka mwenyewe kwa
shehe na kumtaarifu kuhusu hilo
Tayari kijana huyo amekwishafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili
sheria ichukue mkondo.
Tofauti na mbagala hapakuwepo na maandamano wala uharibifu wa mali za
kanisa au msikiti wowote.

Jamani sasa dunia sijui inakoelekea ni wapi, inabidi tuiombee nchi
yetu na kuiepusha na mabalaa haya.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger