Saturday, October 27, 2012
MKE WANGU ANAPENDA KUSHIRIKI KITCHEN PARTY ZA WATU AMBAO HAWAJUI, MULIKA MWIZI!!
Mimi ni mwanamume nina mke na watoto watatu, naipenda sana familia yangu lakini tatizo lipo kwa mke wangu anapenda sana kuhudhuria katika sherehe mbalimbali hakuna sherehe itakayompita kiasi kwamba naona hata kazi anashindwa kufanya inawezekana kila siku yupo kwenye vikao vya kitchen party mara harusi yaani tokea nimemuoa hii tabia imeanza ina mwaka mmoja nimeshawahi kumkalisha chini na kumshauri lakini naona tabia hiyo inaendelea inanikera sana kwani naona hana muda hata wa kukaa na watoto zaidi ya kuwaza sherehe yaani natoa michango ya hizo sherehe majina mengine siyajui ila yeye ananiletea kadi yakutaka mchango nimechoshwa na hii tabia NAOMBENI USHAURI JAMANI. Kwani amekua akitoka kwenda kwenye sherehe kila weekend na kurudi usiku wa manane.
Weka Maoni yako Hapa
0 comments:
Post a Comment