Thursday, October 11, 2012

Linah aja juu baada ya kutuhumiwa kuwa alishawahi kufa na kufufuka!!

http://4.bp.blogspot.com/-4b7RcTYrrW4/UHaL9ya8ujI/AAAAAAAAMpM/RvdGyFNhJG0/s1600/LINAH.jpg
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Estelina Sanga ‘Linah’, amekuja juu akijibu madai kwamba, aliwahi kufa na kufufuliwa na Mchungaji  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa kumfanyia maombi.

Akizungumza na mwandishi wetu, Linah alisema hajawahi kukumbwa na tukio hilo zaidi ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kuzimia mara kwa mara na kuponywa kwa njia ya maombi na Gwajima.

“Kwenye maisha yangu sijawahi kufa na kufufuka, kama umesikia hivyo basi hayo yalikuwa ni maneno tu, hapo mwanzo nilikuwa na kitu kama masheteni yalikuwa yakinikaba na kunifanya nipoteze fahamu mpaka nilipoombewa na Gwajima,” alisema Linah.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger