Ajali za mabasi ya mwendokasi Dar es salaam zimeendelea kumake headlines ambapo leo June 8 2106 mbunge wa viti maalum CCM Amina Mollel
amelifikisha bungeni na kutusaidia kuipata idadi ya mabasi yaliyopata
ajali na kiasi cha fedha zilizotumika kufanya matengenezo.
Amina amesema…’Kwakuwa
ajali nyingi zinasababishwa na madereva wazembe, mfano mzuri ukiwa ni
Dar es salaam ambapo hadi sasa zaidi ya mabasi 30 yamepata ajali na
gharama za matengenezo ikiwa ni zaidi ya milioni 90‘
‘Je, Serikali inatoa kauli gani kuwabana madereva wazembe wanaoisababishia hasara?‘
Majibu yametolewa na Waziri wa ofisi ya Rais tamisemi George Simbachawene ambapo amesema…’Babaraba
zile ni kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi na si vinginevyo, mtumiaji
yoyote anayetumia barabara zile anakuwa amevunja sheria na hivyo yeye
ndio anakuwa amegonga mabasi‘
‘Hawaruhusiwi kutumia barabara za mabasi yaendayo kasi zinazotumika sasa Dar es salaam, niwaombe waheshimu sana barabara hizo‘
0 comments:
Post a Comment