Baada ya Chid Benz kutoka Sober House iliyopo Bagamoyo kwa
ajili ya kupata matibabu ya kuacha kutumia madawa kulevywa, June 16
2016 Chid benz ameeleza jinsi alivyokuwa anaishi katika nyumba ya Sober
House na pia kaweka wazi mipango yake ya kurudi kwenye game ya
bongofleva.
‘Mimi kule nilikuwa naishi
kama staa kwasababu pia wale watu ambao nilikuwa naishi nao walikuwa
wanajua mimi ni mtu ambaye walishawahi kuniona kwenye magazeti na TV kwa
hiyo nilikuwa naishi vizuri hata hivyo Babu Tale aliwambia kuwa wanipe
kipao mbele’ Chid Benz
‘Kuhusu mimi nitakuwa
kwenye lebel gani mimi namuachia Babu Tale kwasababu yeye ndio
aliyeninyanyua upya na kunirudisha niwe kwenye muonekano huu yaani ni
shine kwa mara nyingine, kwahiyo mimi na msikiliza yeye atakachoniambia‘
Chid Benz
0 comments:
Post a Comment