Wednesday, June 15, 2016

Ukatili! Mume Amnyonga Mkewe Hadi Kufa Kisa Kachelewa Kurudi Nyumbani,Shinyanga

MWANAMKE mmoja aliyejulikana kwa jina la Rehema Tumbo amenyongwa hadi kufa na mumewe, Raphael Kazembe kwa kutumia khanga kisa kikuu kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Graiftoni Mushi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na inadaiwa kuwa mwanamke huyo alichelewa kurudi na alipomgongea mumewe huyo chumbani wanakolala hakumfungulia mlango, ndipo alipoamua kwenda kulala kwenye chumba cha watoto.

Baada ya Rehema kulala kwenye chumba hicho cha watoto mumewe huyo aliamua kumfuata na kuanza kumpiga kisha kumnyonga hadi kumuua.

Baada ya mtuhumiwa kutenda unyama huo inadaiwa kuwa alikimbia ambapo mpaka sasa polisi mkoani humo bado wanaendelea na juhudi za kumsaka ili afikishwe kwenye mikono ya sheria.

Aidha Mwenyekiti wa Mtaa huo Bw. Edward Mihayo amesema taarifa zilimfikia kutoka kwa wanamtaa waliomfuata kumwambia mara baada ya kushuhudia maiti ya Rehema ikiwa imenyongwa kwa khanga.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Habari Zinginezo:

0 comments:

Post a Comment

Become a Fan

Popular Posts

Copyright © 2025 GUMZO LA JIJI | Powered by Blogger