Polisi
mkoani Kahama wametumia mabomu ya machozi kutawanya makundi ya wananchi
wanaokutwa wamekusanyika katika maeneo mbalimbali.
Mabomu
hayo yameendelea kurindima katika viwanja vya CDT ili kuwatawanya
wananchi hao waliokusanyika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa hadhara
wa Chadema.
Mkutano
huo ulipangwa kufanyika jana kuanzia saa 9.00 alasiri kabla ya polisi
kuupiga marufuku na jeshi hilo kuzuia mikutano mingine kama hiyo nchini.
Kupitia
taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana jioni na Kamishna
wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Nsato Msanzya amepiga marufuku
maandamano na mikutano ya hadhara hadi hali ya usalama itakapotengemaa.
Amesema Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu yoyote au chama chochote kitakachokaidi agizo hilo.
0 comments:
Post a Comment