Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa mujibu wa Kanuni ya 118 ya Kanuni za
Kudumu za Bunge, Toleo la mwaka 2016, Nyongeza ya Nane, Sehemu ya Tatu
Kifungu cha 9, imepewa jukumu la kusikiliza maoni na mapendekezo ya
wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha kila mwaka.
Katika
kutekeleza jukumu hilo, Kamati ya Bajeti imepanga kufanya Mkutano wa
Wadau wote wa masuala ya kodi (Public Hearing) kwa ajili ya kusikiliza
maoni yao na mapendekezo kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka
2016.
Mkutano
huo umepangwa kufanyika siku ya Alhamisi Tarehe 16 Juni 2016 kuanzia
Saa Tano asubuhi katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Mkoani Dodoma.
Kwa
kuzingatia umuhimu wa Muswada huo, Kamati inawaalika wadau wote kufika
na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine.
Maoni ya wadau yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya Posta au Barua pepe kwa anuani ifuatayo:
Katibu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941,
DODOMA
Barua pepe: cna@bunge.go.tz
Imetolewa na,
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano. Ofisi
0 comments:
Post a Comment