RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,
amesisitiza haja ya kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano uliopo
kati ya Tanzania na Japan.
Alisema
hiyo inatokana na taifa hilo kutambua hatua za nchi hiyo za kuendelea
kuiunga mkono Tanzania katika kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dk Shein alisema hayo jana Ikulu mjini Zanzibar, wakati alipozungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe.
Katika
mazungumzo hayo Dk Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Tanzania ikiwemo
Zanzibar, inajivunia uhusiano na ushirikiano mzuri pamoja na hatua za
Japan za kuendelea kuiunga mkono katika kukamilisha miradi kadhaa ya
maendeleo hapa nchini.
Alisema
Serikali ya Japan pamoja na Shirika lake la Maendeleo la Jica, kwa muda
mrefu zimekuwa zikiunga mkono uimarishaji wa miradi ya maendeleo hapa
nchini, ambapo kwa upande wa Zanzibar nchi hiyo imesaidia mradi mkubwa
wa maji katika Mkoa wa Mjini Magharibi, ambao hivi sasa upo katika awamu
ya tatu.
Dk
Shein pia alitumia fursa hiyo kumueleza Balozi huyo kuwa ipo haja ya
kuitangaza zaidi Tanzania kiutalii kutokana na kuweko vivutio kadhaa
kama fukwe nzuri za bahari kwa Zanzibar na hifadhi za Taifa kwa Tanzania
Bara.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan
Mhe. Mathias M. Chikawe alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kuonana na Rais
0 comments:
Post a Comment