WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuondoka nchini leo jioni (Jumanne,
Mei 10, 2016) kwenda London, Uingereza kuhudhuria mkutano wa wakuu wa
nchi unaojadili suala la kupambana na rushwa (Anti-Corruption Summit
2016) utakaofanyika Mei 12, mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo mchana, Waziri Mkuu amesema anaenda
kumwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli kwa sababu siku
hiyo hiyo, atalazimika kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa
Uganda, Mhe. Yoweri Museveni.
“Mheshimiwa
Dk. Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na
siku hiyo hiyo, mmoja wa marais wa nchi wanachama anaapishwa. Kwa hiyo
amelazimika kwenda kuhudhuria sherehe hizo,” alifafanua Waziri Mkuu.
Akizungumzia
kuhusu mada ya mkutano huo, Waziri Mkuu amesema Tanzania inafanya vema
katika mapambano dhidi ya rushwa na kwamba baadhi ya nchi zimeanza
kuvutiwa na juhudi ambazo Serikali imekuwa ikichukua.
“Waziri
Mkuu wa Uingereza ameandaa mkutano huu na alimwalika Mheshimiwa Rais
Magufuli ili ahudhurie akiwa ni miongoni wa wakuu wa nchi 60
watakaohudhuria mkutano huo. Tanzania ni miongini mwa nchi mbili kutoka
bara la Afrika ambazo zimealikwa kushiriki. Nchi nyingine ya kutoka
Afrika ni Nigeria,” alisema.
Waziri
Mkuu atafuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda, Balozi Dk. Augustine
Mahiga, Mkurugenzi wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola, wataalamu wa
sekta ya rushwa na wanasheria
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU-2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MEI 10, 2016.
0 comments:
Post a Comment