Serikali
imewataka wauzaji wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi (mobile devices)
kuacha mara moja tabia ya kubadilisha namba tambulishi (‘kuflash’) za
vifaa hivyo kwani watakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka 10 au
faini isiyopungua Sh. milioni 30 au vyote viwili.
Kauli
hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy wakati wa mkutano na waandishi wa
habari jana jijini Dar es salaam.
“Namba
tambulishi (IMEI) za vifaa vyote vya mawasiliano ya mkononi ambavyo
vimeibiwa,vimeharibika,kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi
katika soko la mawasiliano havitaruhusiwa kuunganishwa kwenye mitandao
ya watoa huduma ifikapo tarehe 16 June 2016, "alisema Mungy.
Akizungumzia
kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi ya simu zote zisizokidhi
viwango, Mungy alibainisha kuwa idadi ya simu hizo imeshuka kutokana na
elimu ambayo wameitoa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Alisema
lengo la elimu hiyo kwa umma ni kujenga uwezo kwa wananchi kutambua
simu zisizokidhi vigezo kabla ya kufika ukomo wa matumizi ya simu bandia
nchini.
Mungy
alifafanua kuwa uchambuzi wa IMEI unaonyesha kuwa hadi Februari,2016
idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa
na asilimia tatu ambapo namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa
sawa na asilimia 18 na simu halisi zilikuwa sawa na asilimia 79.
“Kwa
mwezi Machi 2016 ulionyesha kuwa Idadi ya namba tambulishi ambazo
hazina viwango ni asilimia nne, na idadi ya zile zilizonakiliwa zilikuwa
sawa na asilimia 13 ambapo uchambuzi huu umehusisha taarifa za kampuni
zote za simu nchini,’’. alifafanua Mungy.
Aliongeza
kuwa matokeo hayo mazuri ni matunda ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya
mamlaka hiyo, Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Tume ya Ushindani
(FCC),kampuni za simu, pamoja na wadau wengine katika kuelimisha umma
juu ya uhakiki wa simu walizonazo ikiwa ni pamoja na mambo muhimu ya
kuzingatia wakati wa kununua simu ikiwemo kuzihakiki ubora wake.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Mawasiliano wa
Mamlaka hiyo, Injinia Gabriel Mruma amesema kuwa ni vyema Watanzania
wakajenga utamaduni wa kununua simu zenye ubora kuepuka usumbufu wakati
Tanzania inapoelekea ukomo wa matumizi ya simu bandia.
TCRA ina dhamana ya kusimamia shughuli za mawasiliano ya Kielektroniki na Posta hapa nchini.
Kuwepo
kwa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka
2010 na kanuni zake za mwaka 2011 kumewezesha kutekelezwa kwa mfumo wa
rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi.
Mfumo
huu wa kielektroniki ulizinduliwa tarehe 17, Desemba 2015 na unahifadhi
kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi kwa
lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vilivyoibiwa,kuharibika
au kupotea,bandia vya mawasiliano katika soko.
0 comments:
Post a Comment