WAZIRI
MKUU wa Norway, Bibi Erna Solberg amemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
ahakikishe Tanzania inatuma wawakilishi wa Serikali kwenye mkutano wa
uwekezaji unaopanga kujadili fursa za uwekezaji barani Afrika
utakaofanyika jijini Oslo, Norway, Oktoba mwaka huu.
Bibi
Solberg ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Mei 12, 2016) alipokutana na
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ya ana kwa ana
kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala
la kupambana na rushwa duniani.
Akizungumzia
kuhusu mkutano huo, Waziri Mkuu wa Norway alisema mkutano huo
umeandaliwa na taasisi binafsi ya Norway Africa Business Association
(NABA) na kwamba anazo taarifa kuwa utalenga kujadili fursa za uwekezaji
barani lakini focus ikiwa ni Tanzania.
“Ni
vema Tanzania ikatuma wawakilishi kwenye mkutano ili waje kuelezea
fursa zilizoko nyumbani. Serikali ilete watu wa kuja kuelezea hali
halisi ikoje nchini Tanzania,” alisema.
Alisema
ili fursa za uwekeaji ziweze kutumika ipasavyo, ni vema Tanzania ikawa
na mfumo wa kimahakama unatoa haki bila upendeleo (a fair judicial
system) kwani utasaidia kujenga hali ya kujiamini kwa wafanyabiasha
wanaokuja kuwekeza Tanzania.
“Mfumo
huu utaleta hamasa kwa wawekezaji, kwani watajua kwamba mitaji yao iko
salama na inalindwa kisheria, hivyo hawatakuwa na hofu,” alisema.
“Hata
hivyo, napenda kusisitiza kuwa makampuni yanayotoka nje na kuja
kuwekeza Tanzania hayana budi kuheshimu sheria za nchi yenu pamoja na za
huku wanakotoka,” alisisitiza.
Akijibu
hoja hiyo, Waziri Mkuu alisema usawa wa kisheria upo nchini kwa sababu
Tanzania imesaini mikataba ya kimataifa ya MIGA na ICSID (International
Centre for Settlement of Investment Disputes) ambayo inahusika na
usuluhishi wa migogoro ya kibiashara.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa alimweleza Bibi Solberg kuwa
Tanzania inahitaji kujifunza kutoka Norway katika suala la uanzishwaji
wa mfuko wa ili mapato yatokanayo na rasilmali za nchi yatunzwe kwa
ajili ya vizazi vijavyo.
Naye
akaipongeza Serikali ya awamu kwa kuanzisha wazo la kutaka kuanzisha
mfuko huo hata kabla ya kuanza kuuza rasilmali hizo. Pia
alimtihibitishia Waziri Mkuu kuwa wao wako tayari kubadilishana uzoefu
na Tanzania katika suala hilo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, MEI 13, 2016.
0 comments:
Post a Comment