Shehena
ya sukari ya kilo milioni 34 zilizokuwa zimefichwa kwenye maghala ya
wafanyabiashara watatu Kilimanjaro imekamatwa na vyombo vya usalama, na
serikali mkoani humo imetangaza kuiuza kwa wananchi kuanzia jana kwa bei
elekezi ya Sh. 1,800.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecki Sadiki alithibitisha jana kukamatwa
kwa shehena hiyo, baada ya makachero wanaoongoza timu maalumu ya ukaguzi
wa maghala ya wafanyabiashara na mawakala wa sukari kubaini kufichwa
kwa bidhaa hiyo.
“Tumefanya ukaguzi katika maghala 45 na katika harakati hizo tumenasa kilo milioni 34 za sukari iliyokuwa imefichwa," alisema.
"Katika
zoezi hilo kuna mfanyabiashara mmoja mkubwa, yeye alikutwa na tani
31.33 lakini alikuwa akiiuza, isipokuwa bado tumewapa kazi Mamlaka ya
Mapato (TRA) ichunguze kama imehodhiwa isivyo halali,” alisema Sadiki.
Kiasi
cha sukari iliyobakia, alisema Mkuu wa M koa huyo, kilikamatwa kwa
wafanyabiashara wengine wawili, ambao walikuwa na tani nne kasoro, Moshi
mjini na Marangu.
Kwa
mujibu wa Mkuu huyo wa mkoa, shehena hiyo ya sukari hadi jana mchana
ilikuwa ikishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kukamilisha
taratibu za kiuchunguzi na kwamba ametoa amri igawiwe kwa wananchi kwa
bei elekezi iliyotangazwa na serikali.
Kuhusu upungufu wa sukari Kilimanjaro, Sadiki alisema "Sisi
kama mkoa tumefanya mawasiliano na mawakala walioko Dar es salaam,
ambao sukari yao ilikuwa inashikiliwa na vyombo vya usalama na
wametuahidi kuukabili uhaba wa sukari uliopo hapa kwetu.
“Jana
(juzi) niliwasiliana na Mmiliki wa Kampuni ya Zakaria Enterprises na
amekubali kuwapa bidhaa hiyo mawakala ambao ni wadau wa Kiwanda cha
Sukari cha TPC," alisema Sadiki.
"Kwa
hiyo tunakwenda vizuri na tumejipanga kuhakikisha kwamba uhaba huo
tunaupatia ufumbuzi wa kudumu.Ila ninawaomba wananchi wangu wawe
wavumilivu kwa sasa.
"Mawakala
wakubwa wa sukari wa Kilimanjaro na mikoa ya Kanda ya Kaskazini ni
mfanyabiashara Vicent Laswai ambaye atapatiwa tani 600 za sukari kutoka
Kampuni ya Zakaria, alisema Mkuu wa Mkoa huyo.
Aidha, Laswai atapokea tani 640 toka katika Kampuni ya Mohamed Enterprises, alisema.
Kampuni
ya Zakaria pia imekubali kutoa tani 640 kwa Kampuni ya Marenga
Investment, alisema Sadiki na kubainisha kuwa Mohamed Enterprises
imemuahidi kuziba pengo la upungufu utakaojitokeza.
Tangu
Rais Magufuli apige marufuku uingizaji sukari kutoka nje ya nchi
Februari 17 mwaka huu, baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu
wamekuwa wakificha bidha hiyo kama njia ya kuihadaa serikali kwamba kuna
uhaba mkubwa.
Wakati
akipiga marufuku, Magufuli alisema kama kutakuwa na uhitaji wa sukari
kuingia nchini, vibali atavitoa yeye si mtu mwingine yeyote ili
kuviwezesha viwanda vya ndani viendelee kuzalisha bidhaa hiyo, kuendelea
kutoa ajira na kuinua kipato cha wakulima wa miwa.
Alisema
inasikitisha kuona sukari ikiingizwa nchini kutoka nje wakati nchi ina
viwanda vingi vya bidhaa hiyo na kusababisha Watanzania wengi kupoteza
ajira kutokana na sukari wanayozalisha kukosa soko.
"Nakuagiza
Waziri Mkuu, kuanzia leo, marufuku mtendaji yeyote wa Serikali kutoa
kibali cha kuagiza na kuingiza sukari kutoka nje ya nchi...vibali vyote
nitatoa mimi," alisema Rais Magufuli.
"Katika
kampeni zangu mwaka 2015, nilisema Serikali yangu itakuwa ya viwanda
hivyo lazima tuvithamini viwanda vya ndani na kulinda bidhaa
zinazozalishwa."
0 comments:
Post a Comment