Upande
wa Jamhuri umekata rufaa kwa mara ya pili katika kesi inayowakabili
Harry Kitilya, Shose Sinare na Sioi Solomoni katika Mahakama ya Rufaa
baada ya rufaa hiyo kukataliwa katika Mahakama Kuu.
Kitilya,
alikuwa Kameshina Mkuu wa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA),
Sinare, Mkuu wa Idara ya ushirikiano na Uwekazaji Katika Benki ya
Stanbic na Sioi, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic
Rufaa
hiyo imekatwa na Buswalo Mganga, Mwendesha mashitaka wa Serikali (DPP)
katika kesi hiyo baada ya kutoridhika na uamuzi wa Mahakama Kuu
ulifanywa wiki iliyopita na Moses Mzuna, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam.
Mganga
alitangaza kukata rufaa mara baada kushindwa pingamizi lao la kupinga
kufutwa kwa shitaka la nane la utakatishaji fedha lililofutwa na Emilis
Mchauru Hakimu Mkazi Kisutu.
Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kutenda makosa saba baada ya kufutwa kosa la nane na kwamba bado watuhumiwa hao wapo lumande.
Jalada
la kesi hiyo lipo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kwamba kesi
hiyo ilipangwa kutajwa tena tarehe 18 Mei mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment